• HABARI MPYA

  Friday, March 15, 2024

  LIVERPOOL NA ATALANTA, WEST HAM NA BAYER LEVERKUSEN ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE


  TIMU ya Liverpool itamenyana na Atalanta ya Italia katika Robó Fainali ya michuano ya UEFA Europa League na ikivuka itakutana na mshindi kati ya Benfica ya Ureno na Marseille ya Ufaransa.
  Hii maana yake inaweza kukutana na vinara wa Bundesliga, Bayer Leverkusen kama wataitoa West Ham ya England pia katika Robó Fainali na mshindi kati ya AC Milan na AS Roma zote za Italia katika Nusu Fainali.
  Droo ya UEFA Europa League imepangwa leo mjini 
  Nyon, Uswisi na mechi za kwanza zitachezwa Aprili 11 na marudiano Aprili 18, wakati Nusu Fainali zitafuatia Mei 2 na Mei 9 na Fainali ni Mei 22 Uwanja wa Aviva Jijini Dublin. 
  RATIBA ROBÓ FAINALI EUROPA LEAGUE:
  1) AC Milan vs Roma
  2) Liverpool vs Atalanta 
  3) Bayer Leverkusen vs West Ham 
  4) Benfica vs Marseille 
  NUSU FAINALI: 
  1) Mshindi Robo Fainali 4 vs Mshindi Robo Fainali  2
  2) Mshindi Robo Fainali 1 vs Mshindi Robo Fainali 3
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL NA ATALANTA, WEST HAM NA BAYER LEVERKUSEN ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top