• HABARI MPYA

  Wednesday, March 06, 2024

  MASHUJAA YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 KIGOMA


  BAO pekee la kiungo Mapinduzi Balama dakika ya saba limeipa Mashujaa FC ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Kwa ushindi huo, Mashujaa FC inafikisha pointi 21 katika mchezo wa 20 na kusogea nafasi ya 11, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 19 za mechi 19 sasa nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHUJAA YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top