• HABARI MPYA

  Saturday, March 09, 2024

  MTIBWA SUGAR YATOKA NYUMA BADO DAKIKA TANO KUICHAPA PRISONS 2-1


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Omar Marungu dakika ya 85 na Seif Abdallah Karihe dakika ya 89, huku bao pekee la Tanzania Prisons likifungwa na Benjamin Asukile dakika ya 45 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar wanafikisha pointi 15 katika mchezo wa 19, ingawa inaendelea kushika mkia, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 27 za mechi 20 sasa nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YATOKA NYUMA BADO DAKIKA TANO KUICHAPA PRISONS 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top