• HABARI MPYA

  Sunday, March 31, 2024

  LIVERPOOL YATOKA NYUMA NA KUICHAPA BRIGHTON 2-1 ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Brighton & Hove Albion walitangulia kwa bao la mshambuliaji Muingereza mwenye asili ya Ghana, Danny Welbeck dakika ya pili, kabla ya Liverpool kutoka nyuma kwa mabao ya washambuliaji wake hodari, Mcolombia Luis Díaz dakika ya 27 na   Mmisri Mohamed Salah dakika ya 65.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 67 katika mchezo wa 29 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi tatu zaidi ya Arsenal inayofuatia ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati Brighton & Hove Albion inabaki na pointi zake 42 za mechi 29 nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATOKA NYUMA NA KUICHAPA BRIGHTON 2-1 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top