• HABARI MPYA

  Friday, March 15, 2024

  LIVERPOOL YATINGA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE KWA KISHINDO


  TIMU ya Liverpool imekamilisha safari yake ya Robo Fainali michuano ya UEFA Europa League baada ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Sparta Prague ya Jamhuri ya Czech usiku wa Alhamisi Uwanja wa  Anfield Jijini Liverpool, England.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Darwin Nunez dakika ya saba, Bobby Clark dakika ya nane, Mohamed Salah dakika ya 10 na Cody Gakpo mawili, dakika ya14 na 55 huku bao pekee la Sparta Prague likifungwa na kiungo Mserbia, Veljko Birmančević dakika ya 42.
  Matokeo haya yanamaanisha Liverpool inaitupa nje Sparta Prague kwa ushindi wa jumla wa mabao 11-2 kufuatia kuichapa 5-1 kwenye mchezo wa kwanza Machi 7 Uwanja wa Epet Arena Jijini Prague.
  Timu nyingine zilizofuzu Robo Fainali ni West Ham United ya England pia, AS Roma, AC Milan, Atalanta za Italia, Benfica ya Ureno, Marseille ya Ufaransa na Bayer Leverkusen ya Ujerumani.
  Droo ya mechi za Robo Fainali itafanyika leo jioni sambamba ya Ligi ya Mabingwa na mechi za kwanza za Nane Bora zitapigwa Aprili 11 na marudiano Aprili 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATINGA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE KWA KISHINDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top