• HABARI MPYA

  Saturday, March 02, 2024

  KMC YATOA SARE NA GEITA GOLD, 1-1 CHAMAZI


  TIMU ya KMC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Geita Gold ilitangulia kwa bao la Yussuf Mhilu dakika ya 45 na ushei, kabla ya Waziri Junior Shentembo kuisawazishia KMC dakika ya 56.
  Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 25 katika mchezo wa 19 na kusogea nafasi ya tano, wakati Geita Gold inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 19 na inashukia nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YATOA SARE NA GEITA GOLD, 1-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top