• HABARI MPYA

  Thursday, March 21, 2024

  EZRA PAUL KUREJEA NA MEDALI YA SHABA ALL AFRICAN GAMES


  BONDIA Ezra Paul Mwanjwango amekuwa mwanamasumbwi wa kwanza wa Tanzania kuandikwa jina lake kwenye orodha ya washindi wa Medali katika Michezo wa Afrika inayoendelea nchini Ghana.
  Ezra amejihakikishia Medali ya Shaba baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Andrew Chilata wa Zambia kwa points za matokeo ya kurejewa 5-2 (Bout review)  baada ya matokeo ya awali 3-2 katika uzito wa Light.
  Mabondia wengine wawili wa Tanzania watapanda ulingoni katika mapambano ya Nusu Fainali ambao ni Nahodha wa timu, Yusuf Changalawe atakayezipiga na Pita Kabejii wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mussa Maregesi atakayepigana na Kanouni O. wa Algeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EZRA PAUL KUREJEA NA MEDALI YA SHABA ALL AFRICAN GAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top