• HABARI MPYA

  Saturday, March 09, 2024

  YUSSUF CHANGALAWE ATUPWA NJE KUFUZU OLIMPIKI


  BONDIA Yusuf Changalawe wa Tanzania ametupwa nje ya mashindano ya kuwania Tiketi ya Olimpiki 20204 Paris, Ufaransa baada ya kuhindwa kwa kwa pointi Mindaugas Gedminas wa Norway katika pambano la uzito wa Light Heavy usiku wa jana mjini Busto Arsizio - Milan, Italia.
  Changalawe aliyeanza vizuri katika Raudi ya kwanza kwa kumshinda Perreira Diego wa Venezuela – sasa ataondoka Itali kwenda Ghana kuungana na timu ya taifa ya Ndondi kwa ajili ya Michezo ya Afrika iliyoanza jana katika miji ya Accra, Kumasi na Cape Coast nchini Ghana.
  Jumla ya mabondia mabondia 50, wanawake 22 na wanaume 28 walitua Italia katika mchujo huo wa kwanza kuwania tiketi ya Olimpiki ambayo itafanyika kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11 Paris na kutakuwa na mchujo wa pili na wa mwisho utakaofuatia Jijini Bangkok nchini Thailand kuanzia Mei 23 hadi Juni 3, ambako huko Tanzania imepanga mabondia wengine 13, wanaume saba, wanawake sita, Changalawe akiwemo.
  Mchujo wa Bangkok nchini Thailand utatoa kati ya mabondia 45 na 51 wa kwenda Olimpiki, kati yao 20 hadi 23 wanawake na 25 hadi 28, wanaume.   • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YUSSUF CHANGALAWE ATUPWA NJE KUFUZU OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top