• HABARI MPYA

  Tuesday, March 12, 2024

  NI SIMBA NA AL AHLY, YANGA NA MAMELODI ROBÓ FAINALI LIGI YA MABINGWA


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC watamenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati watani wao, Simba watamenyana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri.
  Robo Fainali nyingine ni kati ya TP Mazembe ya DRC na Petro Atlético ya Angola na Esperance ya Tunisia dhidi ya ASEC Mimosa ya Ivory Coast.
  Katika Nusu Fainali mshindi kati ya Esperance na ASEC Mimosa 
  atamenyana na mshindi kati ya Yanga SC na Mamelodi na 
  mshindi kati ya TP Mazembe na Petro Atlético atamenyana na mshindi kati ya Simba SC na Al Ahly.
  Katika Kombe la Shirikisho, Modern Future itamenyana na wapinzani wa nyumbani, Zamalek zote za Misri, 
  Abu Salam ya Libya dhidi ya RS Berkane ya Morocco, Rivers United ya Nigeria dhidi ya mabingwa watetezi, USM Alger ya Algeria na Stade Malien ya Mali dhidi ya Dreams FC ya Ghana.
  Katika Nusu Fainali mshindi kati ya 
  Rivers United na USM Alger atakutana na mshindi kati ya Abu Salam na RS Berkane na mshindi kati ya Modern Future na Zamalek atakutana na mshindi kati ya Stade Malien na Dreams FC.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI SIMBA NA AL AHLY, YANGA NA MAMELODI ROBÓ FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top