• HABARI MPYA

    Wednesday, March 13, 2024

    KAMPUNI YA BETPAWA YAINGIA RASMI SIERRA LEONE


    Mkurugenzi wa betPawa nchini Sierra Leone Winifred Boyah akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ofisi mpya ya betPawa nchini Sierra Leone

    KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya betPawa imepanua wigo wake wa  kibishara baada kufungua tawi nchini Sierra Leone.
    Siera Leone inakuwa nchi ya 12 kwa kampuni ya betPawa kufungua matawi yake katika bara la Afrika na kuwawezesha wateja wao kubashiri katika michezo mbalimbali na kujishinda mamilioni ya fedha.
    Sherehe ya utambulisho wa kampuni hiyo ilifanyika kwenye mgahawa wa Lor  mjini Freetown Machi 6, 2024 na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa michezo wa kubashiri ikiwa pamoja na waandishi wa habari.
    Katika halfa hiyo wazungumzaji walikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya  Mchezo (ambayo inamiliki betPawa) Bw Ntoudi Mouyelo, Afisa Mkuu wa Nembo ya betPawa, Spencer Okach, na Mmiliki wa Franchise ya Sierra Leone, Thomas Nsongka wa kampuni ya LionBets & Fastwins Ltd.
    Mbali na kueleza shauku yao ya kukaribishwa nchini Sierra Leone, maofisa hao pia walijadili lengo la betPawa katika michezo ya kubashiri nchini humo.
    Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mchezo, Bw Mouyelo alisema kuwa wamefurahi kuruhusiwa kuingia nchini Sierra Leone ikiwa pamoja na kupata mapokezi makubwa.
     “Dhamira yetu kubwa ni kuufanya mchezo wa kubahatisha kuwa wa burudani na wa urafiki zaidi na wateja wetu watarajie kupata  fursa kubwa ya kufanya biashara na sisi maeneo yote ikiwa pamoja na kasino kama ilivyo katika nchi nyngine 11 za Kiafrika,” alisema Mouyelo.
    Kwa upande wake, Waziri wa Masuala ya Vijana Mohamed Bangura alisema: "Sierra Leone inaikaribisha kwa furaha betPawa na tunatarajia kushirikiana na chapa ya michezo inayotii sheria na inayowajibika mbali na kusaidia ukuaji wa kiuchumi bali pia itasaidia maendeleo ya michezo katika."
    Bw Bangura aliongeza kwa kusema "Uwepo wa betPawa nchini Sierra Leone unaambatana na ahadi ya serikali yetu ya kuunda ajira. Tunatarajia kuwa ushirikiano huu utachangia kwa kiasi kikubwa kufikia lengo letu la kuzalisha ajira 100,000."
    Alisema kuwa betPawa imeonyesha dhamira yake ya uwajibikaji wa kijamii kote Afrika kupitia mipango mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya michezo, udhamini, na huduma za afya.
    Alisema kuwa kuingia katika soko la Sierra Leone, betPawa itaendelea kuchangia pato la taifa ukuwaji wa sekta mbalimbali.
    Kwa upande wake, Thomas Nsongka wa kampuni ya LionBets & Fastwins Ltd alisema kuwa chapa ya betPawa ni rafiki kwa wateja  na wanaamini watafikia malengo yao.
    Alisema kuwa wanadhamira thabiti yenye mahitaji ya kisheria. Kwa mujibu wa Nsongka, nguzo zao muhimu ni kuwawezesha wateja kushiriki katika michezo ya kubahatisha kirafiki zaidi kwa masaa 24 kwa kila siku, malipo ya papo hapo, dau ndogo, na uwezekano wa kushinda kubadilisha maisha na Bonasi ya Ushindi ya asilimia 1000.
    Alisema kuwa haya yanathibitishwa na ushirikiano na waendeshaji wa malipo ya pesa za mkononi kama kampuni ya Orange.
    “Mwezi Oktoba mwaka jana, jumla ya wateja 27,938 walibadili maisha yao ndani ya siku 10 tu na kuwa mabilionea baada ya kujishindia jumla  ya dola za Kimarekani milioni 70 (Sh196.4 billioni) ambazo zililipwa kwa washindi hao.

    Afisa mkuu wa chapa wa betPawa, Spencer Okach (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa betPawa nchini Sierra Leone Winifred Boyah (wa pili kushoto), Waziri wa Masuala ya Vijana Mohamed Bangura (wa pili kulia) na Afisa Mkuu wa Biashara wa betPawa Ntoudi Mouyelo wakishiriki katika uzinduzi wa ofisi ya betPawa nchini Sierra Leone.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMPUNI YA BETPAWA YAINGIA RASMI SIERRA LEONE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top