• HABARI MPYA

  Saturday, March 02, 2024

  CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA BRENTFORD 2-2


  WENYEJI, Brentford FC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Gtech Community mjini Brentford, Middlesex.
  Mabao ya Brentford FC yamefungwa na Mads Roerslev dakika ya 50 na Yoane Wissa dakika ya 69, wakati ya Chelsea yamefungwa na Nicolas Jackson dakika ya 35 na Axel Disasi dakika ya 83.
  Kwa matokeo hayo, Brentford FC wanafikisha pointi 26 katika mchezo wa 27 nafasi ya 15 na Chelsea inafikisha pointi 36 katika mchezo wa 26 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA BRENTFORD 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top