• HABARI MPYA

  Wednesday, March 13, 2024

  JKT TANZANIA NA PRISONS HAKUNA MBABE, SARE 1-1


  TIMU ya JKT Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
  Daniel Lyanga alianza kuifungia JKT Tanzania dakika ya 40, kabla ya mshambuliaji mwenzake, Koplo Samson Baraka Mbangula kuisawazishia Tanzania Prisons dakika ya 46.
  Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya 15 katika Ligi ya timu 16, wakati Tanzania Prisons inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA NA PRISONS HAKUNA MBABE, SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top