• HABARI MPYA

  Thursday, March 21, 2024

  KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA AL AHLY NI SH 5,000 MACHI 29 DAR

  Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam.

  KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Simba SC Ijumaa ya Machi 29 Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam ni Sh. 5,000.
  Afisa Habari wa Simba SC Ahmed Ally ametaja viingilio vingine ni Sh. 10,000 kwa viti vya Rangi ya Chungwa, Sh. 20,000 VIP C, Sh. 30,000 VIP B, Sh. 40,000 VIP A, Sh. 200,000 Platinum na Sh. 250,000 Tanzanite.
  “Tunaamini viingilio hivi ni rafiki kwa kila Mwanasimba. Tunakwenda kucheza mechi dhidi ya Al Ahly, lazima tuelezane ukweli kwamba hii ni mechi ngumu kweli kweli,” amesema Ahmed.
  Simba SC watakuwa wenyeji wa Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali Ijumaa ya Machi 29 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Ijumaa itakayofuata Aprili 5 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo, Misri.
  Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana timu hizo zilikutana katika Robó Fainali ya michuano mipya, African Football League na kutoa sare ya jumla ya 3-3, wakifungana 2-2 Oktoba 20 Dar es Salaam na 1-1 Oktoba 24 Cairo, hivyo Al Ahly kwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini.
  Mshindi wa jumla katí ya Simba na Al Ahly atakutana na mshindi wa jumla katí ya TP Mazembe na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA AL AHLY NI SH 5,000 MACHI 29 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top