• HABARI MPYA

  Saturday, March 16, 2024

  SAMATTA AREJEA UBELGIJI KUWAVAA CLUB BRUGGE ROBÓ FAINALI ULAYA


  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta atarejea Ubelgiji kwa mchezo wa Robó Fainali UEFA Europa Conference League dhidi ya Club Brugge.
  Katika droo ya Robo Fainali za michuano ya klabu Ulaya jana iliyofanyika Jijini Nyon, Uswisi timu ya Samatta, PAOK itaanzia ugenini dhidi ya Club Brugge Aprili 11 kabla ya kurejea Thessaloniki kwa mchezo wa marudiano Aprili 18 Uwanja wa Toumba.
  Mechi nyingine za Robó Fainali UEFA Europa Conference League ni kati ya  Olympiacos ya Ugiriki pia na Fenerbahçe ya Uturuki, Aston Villa ya England na Lille ya Ufaransa na Viktoria Plzeň ya Jamhuri ya Czech na Fiorentina ya Italia.
  PAOK ya Samatta ikiitoa Club Brugge itakutana na mshindi kati ya Olympiacos na Fenerbahçe, wakati mshindi kati ya Olympiacos na Fenerbahçe atakutana na mshindi kati ya Aston Villa na Lille.
  Mechi zote za kwanza za Robó Fainali zitachezwa Aprili 11 na marudiano Aprili 18, wakati Nusu Fainali zitafuatia Mei 2 na Mei 9 na Fainali ni Mei 29 Uwanja wa Agia Sophia Jijini Athens.
  Mbwana Ally Samatta ni mchezaji pekee wa Tanzania aliyecheza michuano yote ya ngazi ya klabu barani Ulaya baada ya awali akiwa na KRC Genk ya Ubelgiji kucheza UEFA Europa League na UEFA Champions League.
  Watanzania wengine waliowahi kucheza michuano ya Ulaya ni Kassim Manara akiwa na SK Klagenfurt ya Austria alicheza iliyokuwa michuano ya UEFA Intertoto mwaka 1984.
  Naye Athumani Machuppa akiwa na Aalborg BK ya Denmark 2008-2009 alicheza Ligi ya Mabingwa na Novatus Dismas wa Shakhtar Donetsk msimu huu Ligi ya Mabingwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AREJEA UBELGIJI KUWAVAA CLUB BRUGGE ROBÓ FAINALI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top