• HABARI MPYA

  Friday, March 22, 2024

  MZIZE AWAKOSAKOSA BULGARIA, TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 BAKU


  TIMU ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeanza vibaya michuano ya FIFA Series baada ya kuchapwa bao 1-0 na Bulgaria leo Uwanja wa 
  Liv Bona Dea Arena Jijini Baku nchini Azerbaijani.
  Bao pekee lililoizamisha Taifa Stars limefungwa na mshambuliaji wa PAOK ya Ugiriki, Kiril Vasilev Despodov kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 52 na kumshinda kipa Kwesi Zion Pira Kawawa anayedakia Orebro Syrianska ya 
  Sweden.
  Kawawa alitokea benchi dakika ya 31 kuchukua nafasi ya Aishi Salum Manula wa Simba SC ya nyumbani aliyeumia na kushindwa kuendelea na mchezo licha ya juhudi za Daktari Lisobin Kisongo kumtibu.
  Naye mshambuliaji wa Yanga, Clement Francis Mzize aliyetokea benchi dakika ya 61 kuchukua nafasi ya Kibu Dennis Prosper wa Simba alikaribia kufunga dakika ya 88 kama si shuti lake kupanguliwa na kipa Dimitar Veselinov Mitov wa St. Johnstone ya Scotland na kwenda juu kidogo ya lango.
  Taifa Stars itashuka tena dimbani Jumatatu kumenyana na Mongolia kuanzia Saa 10:00 jioni katika mchezo wa mwisho wa FIFA Series hapo hapo Liv Bona Dea Arena, wakati Bulgaria itamenyana na Azerbaijan kuanzia Saa 1:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MZIZE AWAKOSAKOSA BULGARIA, TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 BAKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top