• HABARI MPYA

  Tuesday, March 05, 2024

  CHANGALAWE AMCHAKAZA MVENEZUELA KWA KO ROUND YA KWANZA KUFUZU OLIMPIKI


  BONDIA Yusuf Changalawe wa Tanzania amefanikiwa kushinda pambano lake la kwanza kuwania tiketi ya Olimpiki 2024 baada ya kumpiga Pereira Diego wa Venezuela kwa Knockout (KO) dakika ya kwanza ya Raundi ya kwanza uzito wa Light Heavy ukumbi wa E-Work Arena mjini Busto Arsizio, Milan, Italia.
  Kwa ushindi huo, Changalawe amefanikiwa kutinga hatua ya 32 Bora katika mashindano hayo ya kwanza ya Dunia ya kufuzu kushiriki Olimpiki itakayofanyika Jijini Paris nchini Ufaransa kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu. 
  PICHA: Yussuf Changalawe (Kulia) akiwa kazini May, 2023 katika mashindano ya Ubingwa wa Dunia ya IBA yaliyofanyika katika Jiji la Tashkent, Uzbekistan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHANGALAWE AMCHAKAZA MVENEZUELA KWA KO ROUND YA KWANZA KUFUZU OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top