• HABARI MPYA

  Sunday, March 10, 2024

  TANZANIA YAANZA NA SARE DHIDI YA UGANDA ALL AFRICAN GAMES


  TIMU ya taifa ya wasichana U20 jana imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Uganda na Uganda katika mchezo wa kwanza wa Kundi A Michezo ya Afrika jana Uwanja wa Michezo wa Cape Coast Jijini Cape Coast, Ghana.
  Uganda walitangulia kwa bao la Magret Kunihira dakika ya 41, kabla ya Aisha Juma Mnunka kuisawazishia Tanzania dakika ya 89.
  Mechi nyingine ya Kundi A jana, wenyeji Ghana walishinda 1-0 dhidi ya Ethiopia bao pekee la Comfort Owusu dakika ya 58.
  Mechi zijazo, Tanzania itacheza na wenyeji, Ghana Jumanne Saa 5:00 usiku na Uganda na Ethiopia Saa 2:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YAANZA NA SARE DHIDI YA UGANDA ALL AFRICAN GAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top