• HABARI MPYA

  Tuesday, March 26, 2024

  SIMBA SC YAREJEA DAR TAYARI KUMVUA TAJI AHLY IJUMAA


  KIKOSI cha Simba SC kimerejea leo Jijini Dar es Salaam kutoka visiwani Zanzíbar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly.
  Simba iliweka kambi ya wiki moja visiwani Zanzíbar kujiandaa na mechi hiyo itakayofanyika Ijumaa kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Timu hizo zitarudiana Ijumaa ya wiki ijayo, Aprili 5 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo, Misri na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya TP Mazembe na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali.
  Ikumbukwe timu hizo zilikutana katika Robó Fainali ya michuano mipya, African Football League na kutoa sare ya jumla ya 3-3, wakifungana 2-2 Oktoba 20 Dar es Salaam na 1-1 Oktoba 24 Cairo, hivyo Al Ahly kwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini.
  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAREJEA DAR TAYARI KUMVUA TAJI AHLY IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top