• HABARI MPYA

  Saturday, March 30, 2024

  CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA BURNLEY PUNGUFU STAMFORD BRIDGE


  WENYEJI, Chelsea FC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Burnley FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Chelsea leo yote yamefungwa na kiungo mshambuliaji. Cole Palmer kwa penalti dakika ya 44 na dakika ya 78 akimalizia pasi ya nyota mwenzake wa England, mshahara Raheem Sterling.
  Kwa upande wao Burnley FC mabao yao yamefungwa na Joshua Cullen dakika ya 47 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake, Joshua Brownhill na beki Dara O'Shea dakika ya 81 akimalizia pasi ya mfungaji wa bao lao la kwanza.
  Burnley FC ilimaliza pungufu baada ya beki wake Mfaransa, Lorenz Assignon kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 40 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
  Ikawa siku mbaya zaidi kwao baada ya Kocha wake pia, Vincent Kompany kutolewa pia kwa kadi nyekundu baada ya kutofautiana kauli na waamuzi.
  Matokeo hayo yanaifanya Chelsea ifikishe pointi 40 katika mchezo wa 28 na kusogea nafasi ya 11, wakati Burnley inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 30, ingawa inabaki nafasi ya 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA BURNLEY PUNGUFU STAMFORD BRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top