• HABARI MPYA

  Saturday, March 09, 2024

  MAN UNITED YAWACHAPA EVERTON 2-0 OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao yote ya Manchester United yamewekwa kimiani kwa mikwaju ya penalti, la kwanza kiungo Mreno Bruno Fernandes dakika ya 12 na la pili mshambuliaji Muingereza, Marcus Rashford dakika ya 36.
  Kwa ushindi huo, Manchester United wanafiisha pointi 47 na kusogea nafasi ya sita, wakati Everton inabaki na pointi zake 25 nafasi ya 16 baada ya wote kucheza mechi 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAWACHAPA EVERTON 2-0 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top