• HABARI MPYA

  Monday, March 25, 2024

  TAIFA STARS YAICHAPA MONGOLIA 3-0 LEO BAKU


  TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mongolia katika mchezo wa Mashindano mapya ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), yanayojulikana kama FIFA Series leo Uwanja wa  Liv Bona Dea Arena mjini Baku nchini Azerbaijani.
  Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na washambuliaji Kelvin Pius John wa KRC Genk II dakika ya 49, Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ wa Azam FC dakika ya 62 na kiungo wa Shakhtar Donetsk, Novatus Dissmas Miroshi dakika ya 76.
  Huo ulikuwa mchezo wa pili kwa Taifa Stars kwenye michuano hiyo baada ya Machi 22 kufungwa 1-0 na Bulgaria hapo hapo Liv Bona Dea Arena.
  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAICHAPA MONGOLIA 3-0 LEO BAKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top