• HABARI MPYA

  Friday, March 29, 2024

  MAMELODI SUNDOWNS WAWASILI DAR KUIKABILI YANGA SC KESHO


  KIKOSI cha Mamelodi Sundowns kimewasili usiku wa kuamkia leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Yanga SC.
  Kundi liliotua jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ni la pili ambalo ndilo kubwa, baada ya kikundi cha wachezaji sita waliokuwa na timu ya taifa, Bafana Bafana kutangulia kuwasili juzi.
  Mamelodi Sundowns watakuwa wageni wa Yanga kesho kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana  Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria.
  Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2001 na Mamelodi Sundowns wakaitoa Yanga kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 3-2 Pretoria na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mshindi wa jumla baina ya Yanga na Mamelodi Sundwons atakutana na mshindi wa jumla katí ya Esperance ya Tunisia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
  TAZAMA VÍDEO MAMELODI SUNDOWNS WAKIWASILI JNIA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMELODI SUNDOWNS WAWASILI DAR KUIKABILI YANGA SC KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top