• HABARI MPYA

    Saturday, March 16, 2024

    BONDIA WA KWANZA WA TANZANIA ATOLEWA ALL AFRICAN GAMES

    AJALI ya kuvunjika mkono katika round ya mwisho ya mchezo imemuondoa katika mashindano bondia Abdallah Abdallah "Katoto" aliyekuwa akipambana na Wibshet Bekele kutoka Ethiopia.
    Ilikua katika bout no. 3 ya hatua ya 16 bora ya mashindano hayo katika uzani wa Fly weight 51kg ambapo Katoto alipata ajali hiyo akijiandaa kufanya shambulizi dhidi ya mpinzani wake katika round ya 3 na ya mwisho ambapo alipata ajali hio na kumlazimu mwamuzi wa mchezo kusimamisha pambano na Katoto kupelekwa moja kwa moja hospital kwa ajili ya matibabu.
    "Katoto tulimwahisha kwenda University of Ghana Medical Center kwa ajili ya matibabu na baada ya kuchukuliwa vipimo alionekana amevunjika sehemu ya katikati ya mkono, ila tunashukuru Mungu hali yake binafsi inaendelea vizuri ingawa hatoweza kucheza kwa kipindi cha karibuni" alisema Muhsini Mng'ola, mwalimu msaidizi wa timu ya Taifa ya ngumi.


    Abdallah Katoto (kulia) akiwa na Kocha Mkuu, Samuel Kapungu kwenye matibabu Kituo cha Tiba cha Chuo Kikuu cha Ghana.

    Baada ya pambano hilo Katoto alikua apambane hatua ya robo fainali dhidi ya Patrick Chinyemba wa kutoka Zambia ambaye ni Bingwa wa Afrika na tayari ameshakata tiketi ya kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024.
    "Ndoto yangu kubwa sana ilikua katika pambano langu la robo fainali dhidi ya Chinyemba wa Zambia na kutaka kuishangaza Afrika na Dunia kwa uwezo wangu, pambano hili la muethiopia nilikua nauhakika na ushindi kwa maandalizi mazuri tuliyoyapata" alisema Katoto.
    Bondia huyo machachari kama kawaida yake alikua ameshajizolea idadi kubwa ya mashabiki katika ukumbi wa Bukom Arena kwa aina ya uchezaji wake wenye mvuto mkubwa kwa mashabiki.
    Naye Raisi wa Shirikisho, Lukelo Willilo alisema "Tunamshukuru Mungu kwa yote, ndio mchezo ulivyo, zilikua zimebaki sekunde chache pambano liishe huku tukiongoza kwa matokeo, lakini mchezo wakati mwingine una matokeo katili"
    Wakati huo huo, session ya 2 ya mapambano ya jana ilihairishwa mpaka leo jioni ambapo bondia wetu Abdallah Mfaume "Nachoka" alikua apambane na Gerald Kabinda kutoka Zambia katika hatua ya 16 bora uzani wa Welterweight. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BONDIA WA KWANZA WA TANZANIA ATOLEWA ALL AFRICAN GAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top