• HABARI MPYA

  Sunday, March 17, 2024

  FEI TOTO AFUNGA LA USHINDI AZAM YAILAZA YANGA 2-1


  TIMU ya Azam FC imetoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize alianza kuifungia Yanga dakika ya 10, kabla ya Azam FC kutokea nyuma kwa mabao ya winga Mgambia, Gibrill Sillah dakika ya 19 na kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah dakika ya 51.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 47 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na Yanga ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Vigogo wengine katika mbio za ubingwa, Simba SC wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 45 za mechi 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEI TOTO AFUNGA LA USHINDI AZAM YAILAZA YANGA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top