• HABARI MPYA

    Tuesday, March 12, 2024

    AZAM FC YAINGIA MIKATABA NA ‘AKADEMI’ KIBAO MIKOANI


    KLABU ya Azam FC imeingia makubaliano ya ushirikiano na vituo nane vya kulea vipaji (academies) za mikoa mbalimbali nchini.
    Taarifa ya Azam FC imesema kwamba Vituo hivyo nane vitakuwa ni 'AZAM FC CENTERS', vikiiwakilisha klabu hiyo katika mikoa husika, vikiwa na jukumu la kutafuta vipaji vya wachezaji vijana wa Kitanzania, watakaokuja kujiunga na Azam FC Academy kutokana na mahitaji ya timu yetu.
    Taarifa imevitaja vituo hivyo ni JK7Pro Football Center (Tanga), Tutes Hub Sports Center (Songea), Maendeleo Youth Sports Center (Mtwara), Kilwa Youth Sports Center (Lindi), Muleba Youth Sports Center (Kagera), Mwanga City Sports Center (Kigoma), Rungwe Youth Sports Center (Mbeya) na Korogwe Youth Soccer Center (Korogwe).
    Azam FC imesema itavipa kipaumbele vituo hivyo katika kuvuna vipaji vya vijana wakihitaji wachezaji kwenye kituo chao, Azam Academy.
    “Lakini sisi kama Azam FC tunaothamini vipaji vya vijana wadogo, tutaendelea na jukumu letu la kila mara la kuvuna vipaji popote pale nchini, tukiendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika juhudi zake za kukuza maendeleo ya michezo nchini,”imesema taarifa ya Azam FC na kuongeza;
    “Tayari makubaliano kati ya vituo vyote hivyo na Azam FC yameingiwa kwa mikataba rasmi, zoezi lililosimamiwa kwa ukaribu na Vice Chairman, Omary Kuwe,”.
    “Mara baada ya zoezi hilo kukamilika, hivi karibuni benchi letu la timu za vijana, litatembelea vituo hivyo (Azam FC Centers) kwa ajili ya kukutana na makocha wanaofundisha vijana hao, lengo likiwa ni kuwajenga zaidi na kuwapa vigezo vya aina ya wachezaji wanaowahitaji,”.
    “Kwa kuanzia, tumeanza na vituo hivyo nane, lakini katika ramani yetu tumepanga kuifikia Tanzania nzima kwa kuwa na 'Azam Centers' katika mikoa yote nchini,”.
    “Tunaamini kuwa kupitia programu hii, klabu yetu itaweza kuvuna vipaji bora vya vijana wa Kitanzania na kuviendeleza zaidi pale watakapofika kwenye kituo chetu 'Azam FC Academy',” imemalizia taarifa hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAINGIA MIKATABA NA ‘AKADEMI’ KIBAO MIKOANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top