• HABARI MPYA

  Tuesday, March 12, 2024

  NTIBANZOKIZA APIGA MBILI SIMBA SC YAICHAPA SINGIDA 3-1


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza mawili, dakika ya sita na la penalti dakika ya tisa na mshambuliaji Muivory Coast, Freddy Michael Koublan dakika ya 34, wakati bao pekee la Singida FG limefungwa na mshambuliaji mzawa, Thomas Ulimwengu dakika ya 84.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 39 katika mchezo wa 18, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi tano na Azam FC ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi.
  Kwa upande wao Singida Fountain Gate wanabaki na pointi zao 21 za mechi sasa na wanashuka kwa nafasi moja hadi ya 12 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kwenye mchujo wa kuwania kusalia Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NTIBANZOKIZA APIGA MBILI SIMBA SC YAICHAPA SINGIDA 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top