• HABARI MPYA

  Sunday, March 31, 2024

  MANCHESTER UNITED YAAMBULIA SARE 1-1 KWA BRENTFORD


  TIMU ya Manchester United imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Gtech Community mjini Brentford, Middlesex.
  Manchester United walitangulia kwa bao la Mason Mount dakika ya  90'+6, kabla ya Kristoffer Ajer kuisawazishia Brentford dakika ya  90'+9.
  Kwa matokeo hayo, Manchester United inafikisha pointi 48 katika mchezo wa 29, ingawa inabaki nafasi ya sita, wakati Brentford inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 30 na kusogea nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER UNITED YAAMBULIA SARE 1-1 KWA BRENTFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top