• HABARI MPYA

  Saturday, March 09, 2024

  ARSENAL YAICHAPA BRENTFORD 2-1 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND


  WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na viungo, Muingereza Declan Rice dakika ya 19 na Mjerumani, Kai Havertz dakika ya 86, huku bao pekee la Brentford  likifungwa dakika ya kiungo Mkongo mzaliwa wa Ufaransa, Yoane Wissa Bileko dakika ya 45 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 64 katika mchezo wa 28 na kurejea kileleni mwa Ligi, ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 63 na Manchester City pointi 62 baada ya wote kucheza mechi 27.
  Kwa upande wao, Brentford baada ya kipigo cha leo inabaki na pointi zake 26 za mechi 28 sasa nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA BRENTFORD 2-1 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top