• HABARI MPYA

  Tuesday, March 19, 2024

  TANZANIA YAJIHAKIKISHIA MEDALI MBILI NDONDI ALL AFRICAN GAMES


  BONDIA Ezra Paul Mwanjwango wa Tanzania amefanikiwa kutinga Nusu Fainali katika Michezo ya Afrika (All African Games) inayoendelea nchini Ghana baada ya kumshinda Mujinga Frazier wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa pointi 5-0 katika uzito wa Light ukumbi wa Bukom Arena Jijini Accra.
  Kwa ushindi huo, Ezra Paul Mwanjwango amejihakikishia Medali ambayo inakuwa ya pili kwa timu ya taifa ya Tanzania  ya Ndondi za Ridhaa ‘Faru Weusi wa Ngorongoro’ baada ya Mussa Maregesi wa uzito wa Cruiser.
  Katika Nusu Fainali, Ezra Paul Mwanjwango atakutana na Andrew Chilata wa Zambia na hata kama atapoteza tayari ana uhakika wa kupata Medali ya Shaba, ambayo hutolewa kwa wana Nusu Fainali wote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YAJIHAKIKISHIA MEDALI MBILI NDONDI ALL AFRICAN GAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top