• HABARI MPYA

  Sunday, March 17, 2024

  CHELSEA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND


  WENYEJI, Chelsea wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Leicester City leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na Marc Cucurella dakika ya 13, Cole Palmer dakika ya 45'+1, Carney  Chukwuemeka dakika ya 90'+2 na 
  Noni Madueke dakika ya 90'+8 ,  wakati ya Leicester City yamefungwa na Axel Disasi aliyejifunga dakika ya 51 na Stephy Mavididi dakika ya 62.
  Haikuwa siku nzuri kwa Raheem Sterling wa Chelsea aliyekosa penalti dakika ya 27, kabla ya Callum Doyle wa Leicester City kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 73 kwa kumchezea rafu Nicolas Jackson.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top