• HABARI MPYA

    Saturday, March 23, 2024

    NDONDI ZAITOA KIMASOMASO TANZANIA ALL AFRICAN GAMES 2024


    Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Anderson Lukelo Willilo (aliyevaa suti) katika picha ya pamoja na washindi wa Medali na wenzao. 

    TIMU ya Taifa ya Ngumi ya Tanzania ‘Faru Weusi wa Ngorongoro’ imefanikiwa kuiheshimisha Tanzania katika michezo ya 13 ya Afrika inayofikia tamati usiku wa leo katika Jiji la Accra, Ghana.
    Timu hiyo imefanikiwa kushinda medali 3 za shaba katika mashindano hayo kutoka kwa wachezaji Light Heavyweight Yusuf Changalawe (Nahodha), Lightweight Ezra Paulo Mwanjwango na Cruiserweight Musa Maregesi. 
    Wachezaji wote hao wanatokea katika Klabu ya Ngome inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
    Katika sherehe za utoaji wa medali kwa washindi katika mchezo wa ngumi iliyofanyika jana usiku katika ukumbi wa Bukom Arena, Raisi wa Shirikisho la Ngumi Tanzania na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Shirikisho la Ngumi la Bara la Afrika (AFBC) alipata kuwa mgeni rasmi katika kuwavalisha washindi wa Uzani wa Ligh Heavyweight 80kg kwa Wanaume na Cruiserweight 86kg ambapo Changalawe na Maregesi walikuwa moja ya washindi katika uzani hizo.
    Kikosi hicho cha Faru Weusi wa Ngorongoro pamoja na wachezaji wa michezo mingine walioiwakilisha Timu Tanzania katika michezo hiyo, wanatarajia kurejea Dar es salaam kesho saa 9.40 usiku kwa Shirika la Ndege la Ethiopia kupitia Addis Ababa. 
    Kikosi hicho kikirejea Tanzania kitaendelea na mazoezi kujiandaa kushiriki mashindano ya Mandela *"Mandela Cup"* yatakayofanyika Durban, Afrika ya Kusini kuanzia tarehe 15-23 April, 2024.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDONDI ZAITOA KIMASOMASO TANZANIA ALL AFRICAN GAMES 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top