• HABARI MPYA

    Wednesday, March 20, 2024

    BETPAWA YATOA MABILIONI YA FEDHA KUDHAMINI TIMU ZA TAIFA ZA KIKAPU UGANDA


    Maafisa wa kamati ya timu za Taifa wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Uganda (FUBA), watendaji wa betPawa na wawakilishi wa timu mbili za kitaifa za mpira wa kikapu  za wanaume na wanawake wakiwa katika picha ya pamoja  baada ya sherehe ya kusaini mkataba wa udhamini.

    TIMU za taifa za mpira wa kikapu za  wanaume (Silverbacks) na wanawake (Gazelles) zimepata udhamini mnono kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri ya betPawa wenye thamani ya sh2.6 bilioni za Uganda, sawa n ash Bilioni 1.8 za Kitanzania.
    Mkataba wa udhamini huo wa miaka mitatu ulisainiwa jana kati ya maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Uganda (FUBA) na viongozi wa ngazi za juu wa betPawa.
    Mbali ya kugharimia timu hiyo katika michezo mbalimbali ya kimataifa, betPawa pia itagharimia kambi ya timu, usafiri, malazi, gharama za kushiriki katika mashindano mbalimbali, bifa ya afya na mambo mengine muhimu za timu hizo.
    Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, Afisa Mkuu wa Chapa wa betPawa, Spencer Okach alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kuchangia maendeleo ya michezo nchini Uganda.
    "Lengo letu ni kuhakikisha  Uganda inapata maendeleo makubwa katika mpira wa kikapu na michezo kwa ujumla ndiyo maana tumeingia mkataba mkubwa wa udhamini,” alisema Okach.
    Alisema kuwa kupitia udhamini huo, betPawa pia italipa moja kwa moja kiasi cha Sh150,000 za Uganda (Sh98,000) za Tanzania kama bonasi ya ushindi kwa kila mchezaji wa timu ya taifa ya Uganda. Bonasi hiyo ni kwa ushindi kwa mechi.
    Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa FUBA, Marcus Kwikiriza aliipongeza kampuni ya betPawa kwa udhamini huo mnono kwani umeweka historia.
    "Hii ni mara ya kwanza wachezaji wetu wanapata motisha ambapo kampuni binafsi ya betPawa  inadhamini timu ya kitaifa ya mpira wa kikapu,” alisema Kwikiriza.
    Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Idara ya Michezo wa Uganda, Peter Ogwang alipongeza betPawa kwa udhamini huo akibainisha kuwa katika nchi nyingi michezo inasaidiwa zaidi na sekta binafsi.
    Ogwang alisema kuwa anatarajia timu hizo za taifa kufanya vizuri zaidi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.
    "Ni faraja kubwa na wadhamini wanastahili pongezi kubwa. Matatizo yanayokabili michezo yanaweza kutatuliwa tu na washirika tulionao hapa. Mahali pengine, wadhamini binafsi wanakuwa na jukumu kubwa katika kusaidia timu. Asante kwa betPawa kwa kuleta changamoto hapa," alisema.
    Naye Meneja na msimamizi wa timu hizo, Albert Ahabwe alisema maendeleo ya timu  zao awali yaliathiriwa na matatizo ya kifedha pamoja na kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu.
    Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Biashara wa betPawa, Ntoudi Mouyelo alisema kuwa kampuni yao ina mipango mikubwa ikiwa pamoja na kuwa ya kwanza barani Afrika.
    Mouyelo alisema udhamini wao umekuwa wa wakati muafaka kutokana maendeleo makubwa ya mpira wa kikapu na Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Afrika (BAL).
    Alisema ushirikiano wao na FUBA utaleta maendeleo chanya ya mchezo huo hasa kwa wachezaji na klabu  kwani betPawa itawawezesha kushindana katika michezo mbalimbali.
    “Timu ya wanaume (Silverbacks) imetajwa na Shirikisho la mpira wa kikapu duniani (FIBA) kuwa moja ya timu ambayo imepanda katika viwango kwa nafasi nne mpaka kufikia ya 83 kati ya nchi 160. Haya ni maendeleo makubwa, udhamini wetu huu utasaidia kupanda chati zaidi duniani,” alisema.

    Afisa Mkuu wa Biashara wa betPawa Ntoudi Mouyelo akizungumza katika hafla hiyo.


    Afisa Mkuu wa Chapa (Brand) wa betPawa, Spencer Okach, akizungumza katika hafla hiyo.
    Waziri wa michezo wa Uganda Peter Ogwang akizungumza katika hafla hiyo
    Katibu Mkuu wa baraza la michezo la Uganda Bernard Ogwe akizungumza katika hafla hiyo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BETPAWA YATOA MABILIONI YA FEDHA KUDHAMINI TIMU ZA TAIFA ZA KIKAPU UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top