• HABARI MPYA

  Tuesday, March 19, 2024

  YANGA YAANZA KUJIFUA KIGAMBONI KUIKUSANYIA NGUVU MAMELODI


  KIKOSI cha Yanga SC leo kimeingia kambini, Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kujiandaa na michezo miwili ya nyumbani na ugenini Robó Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
  Yanga watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns Jumamosi ya Machi 30 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana  Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria.
  Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2001 na Mamelodi Sundowns wakaitoa Yanga kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 3-2 Pretoria na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAANZA KUJIFUA KIGAMBONI KUIKUSANYIA NGUVU MAMELODI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top