• HABARI MPYA

  Monday, March 25, 2024

  MWANACHAMA MKONGWE YANGA, MZEE MANENO AFARIKI DUNIA DODOMA


  MWANACHAMA wa muda mrefu wa Yanga na aliyekuwa mfanyakazi wa klabu hiyo, Meneno Hussein amefariki dunia leo nyumbani kwao Jijini Dodoma baada ya kusumbuliwa na maradhi.
  Maneno alifahamika Yanga miaka ya 1980 akianza kama mpenzi aliyejitolea kusaidia timu kifedha, kabla ya baadaye kupangishwa eneo la biashara ya vinywaji makao makuu ya klabu, Jangwani.
  Kufuatia kufungwa kwa Kaunta ya vinywaji klabuni, Maneno akahamia kwenye utumishi wa klabu kwanza kwa kujitolea kama mmoja msimamizi wa mapato na baadaye kuajiriwa kama mlinzi wa kambi ya timu.
  Mungu ampumzishe kwa amani Maneno Hussein. Amín.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWANACHAMA MKONGWE YANGA, MZEE MANENO AFARIKI DUNIA DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top