• HABARI MPYA

  Wednesday, March 13, 2024

  TANZANITE YAFUNGWA 2-1 NA GHANA ALL AFRICAN GAMES


  TIMU ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite jana imefungwa mabao 2-1 na wenyeji, Ghana katika mchezo wa Kundi A Michezo ya Afrika (All African Games) Uwanja wa Michezo wa Jiii la Cape Coast.
  Kwa ushindi wa jana Ghana wanafuzu Nusu Fainali kabla ya mechi ya mwisho dhidi ya Uganda, wakati Tanzania inabaki na pointi moja na italazimika kushinda dhidi ya Ethiopia kwenye mechi ya mwisho kujaribu kwenda Nusu Fainali.
  Ghana inaongoza kwa pointi zake sita ikifuatiwa na Uganda ambayo jana imeifunga Ethiopia 2-0, Tanzania ya tatu pointi moja na Wahabeshi wanashika mkia hawana pointi.
  Ili kwenda Nusu Fainali, Tanzanite itatakiwa kuifunga Ethiopia si chini ya Mabao 3-0 na iombe Uganda nayo ifungwe na Ghana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YAFUNGWA 2-1 NA GHANA ALL AFRICAN GAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top