• HABARI MPYA

  Thursday, March 14, 2024

  MUDATHIR YAHYA MCHEZAJI BORA WA YANGA FEBRUARI


  NYOTA Mudathir Yahya Abbas ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Yanga SC kwa mwezi Februari akiendeleza mwanzo mzuri wa mwaka huu kwa wazawa, baada ya mshambuliaji Clement Francis Mzize kushinda tuzo ya Januari.
  Mudathir ameshinda kiungo mwenzake, Muivory Coast, Peodoh Pacôme Zouzoua na beki mzawa mwenzake, Nickson Clement Kibabage alioingia Fainali.
  Kwa kushinda Tuzo hiyo, Mudathir atazawadiwa kitita cha Sh. Milioni 3 kutoka kwa wadhamini, kampuni ya NIC Insurance.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUDATHIR YAHYA MCHEZAJI BORA WA YANGA FEBRUARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top