• HABARI MPYA

  Tuesday, March 19, 2024

  SIMBA SC YAINGIA KAMBINI ZANZÍBAR KUJIANDAA NA AL AHLY


  KLABU ya Simba leo imeingia kambini visiwani Zanzíbar kujiandaa na mechi mbili za nyumbani na ugenini Robó Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly.
  Simba SC watakuwa wenyeji wa Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali Ijumaa ya Machi 29 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Ijumaa itakayofuata Aprili 5 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo, Misri.
  Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana timu hizo zilikutana katika Robó Fainali ya michuano mipya, African Football League na kutoa sare ya jumla ya 3-3, wakifungana 2-2 Oktoba 20 Dar es Salaam na 1-1 Oktoba 24 Cairo, hivyo Al Ahly kwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAINGIA KAMBINI ZANZÍBAR KUJIANDAA NA AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top