• HABARI MPYA

  Tuesday, March 05, 2024

  ARSENAL YAITANDIKA SHEFFIELD UNITED 6-0 BRAMALL LANE


  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya wenyeji, Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Bramall Lane mjini Sheffield.
  Mabao ya Arsenal yalifungwa na Martin Odegaard dakika ya tano, Jayden Bogle aliyejifunga dakika ya 13, Gabriel Martinelli dakika ya 15, Kai Havertz dakika ya 25, Declan Rice dakika ya 39 na Ben White dakika ya 58.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 61, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Manchester City pointi 62 na Liverpool pointi 63 baada ya wote kucheza mechi 27, wakati Sheffield United inaendelea kushika mkia na pointi zake 13 za mechi 27 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAITANDIKA SHEFFIELD UNITED 6-0 BRAMALL LANE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top