• HABARI MPYA

  Saturday, March 16, 2024

  SINGIDA FOUNTAIN GATE YAZINDUKA CHINI YA JULIO, YAICHAPA NAMUNGO 1-0


  TIMU ya Singida Fountain Gate imezinduka kwa kuichapa Namungo FC 1-0, bao pekee la beki Mghana, Nicholas Gyan dakika y 15 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Kwa ushindi huo wa kwanza ndani ya mechi 10 Singida Fountain Gate inafikisha pointi 24 na kupanda nafasi ya saba, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 23 na inashukia nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 21.
  Mechi tisa zilizopita, Singida Fountain Gate imepoteza sita, 0-1 Geita Gold, 0-1 Kagera Sugar, 1-3 Tanzania Prisons, 0-1 Azam FC, 0-2 Mtibwa Sugar na 1-3 Simba SC na kutoa sare tatu, 2-2 JKT Tanzania, 0-0 KMC na 1-1 Tabora United.
  Baada ya mechi nane za bila kushinda Singida walimfukuza Kocha Thabo Senong raia wa Afrika Kusini na mzawa, Ngawina Ramadhani akaiongoza timu kufungwa 3-1 na Simba, kabla ya kocha maarufu mzawa, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kupewa madaraka na leo wamezinduka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA FOUNTAIN GATE YAZINDUKA CHINI YA JULIO, YAICHAPA NAMUNGO 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top