• HABARI MPYA

  Saturday, March 09, 2024

  JOSHUA AMTWANGA NGANNOU KWA KO RAUNDI YA PILI


  BINGWA mara mbili wa dunia wa ngumi za kulipwa, Muingereza Anthony Joshua usiku wa jana amemshinda kwa Knockout (KO) raundi ya Pili tu, Mfaransa mzaliwa wa Cameroon, Francis Ngannou katika pambano la uzito wa juu ukumbi wa Kingdom Arena, Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
  Hilo lilikuwa pambano la pili tu kwa Ngannou (37), bingwa wa zamani wa uzito wa juu wa UFC baada ya kupoteza kwa pointi za majaji wawili kwa mmoja dhidi ya Muingereza mwingine, Tyson Fury Oktoba mwaka jana, ingawa siku hiyo alimuangusha bingwa huyo wa WBC katika raundi ya tatu.
  Joshua (34), mwenye asili ya Nigeriaa ambaye ni bingwa wa zamani wa WBO, WBA na IBF uzito wa juu, hilo linakuwa pambano la nne mfululizo kushinda baada ya kupigwa mara mbili mfululizo na Oleksandr Usyk wa Ukraine, ambaye atazipiga na Fury kumtafuta bingwa asiyepingika wa uzito wa juu Mei mwaka huu hapo hapo Saudi Arabia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOSHUA AMTWANGA NGANNOU KWA KO RAUNDI YA PILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top