• HABARI MPYA

  Sunday, March 17, 2024

  MANCHESTER CITY YAICHAPA NEWCASTLE UNITED 2-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI FA


  TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la FA England kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle United mabao ya Bernardo Silva dakika ya 13 na 31 jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mapema katika mchezo uliotangulia jana nayo Coventry City ilitinga Nusu Fainali pia kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Wolverhampton Wanderers Uwanja wa Molineux mjini Wolverhampton, West Midlands.
  Robo Fainali za mwisho za Kombe la FA England zinapigwa leo; Chelsea na Leicester City Saa 9:45 Alasiri Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London na Manchester United dhidi ya Liverpool Saa 12:30 jioni Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAICHAPA NEWCASTLE UNITED 2-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top