• HABARI MPYA

  Sunday, March 10, 2024

  LIVERPOOL NA MAN CITY NGOMA DROO, 1-1 ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa watetezi, Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Beki Muingereza John Stones alianza kuifungia Manchester City dakika ya 23 akimalizia pasi ya kiungo Mbelgiji Kevin De Bruyne, kabla ya kiungo Muargentina Alexis Mac Allister kuisawazishia Liverpool kwa penalti dakika ya 50 kufuatia kipa Mbrazil, Ederson Santana de Moraes kumchezea rafu mshambuliaji wa Uruguay, Darwin Núñez dakika ya 47.
  Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 64, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na Arsenal, wakati Manchester City inafikisha pointi 63 na inabaki nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL NA MAN CITY NGOMA DROO, 1-1 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top