• HABARI MPYA

  Wednesday, March 27, 2024

  AL AHLY TAYARI WAPO DAR KUIKABILI SIMBA IJUMAA

   

  KIKOSI cha Al Ahly ya Misri kimewasili mchana huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Simba SC.
  Mabingwa hao watetezi, Al Ahly watakuwa wageni wa Simba Ijumaa kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Aprili 6 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo.
  Mshindi wa jumla katí ya Simba SC na Al Ahly atakutana na mshindi wa jumla katí ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali.
  Ikumbukwe timu hizo zilikutana katika Robó Fainali ya michuano mipya, African Football League na kutoa sare ya jumla ya 3-3, wakifungana 2-2 Oktoba 20 Dar es Salaam na 1-1 Oktoba 24 Cairo, hivyo Al Ahly kwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini.
  GONGA KUTAZAMA VÍDEO AHLY WAKIWASILI DAR
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY TAYARI WAPO DAR KUIKABILI SIMBA IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top