• HABARI MPYA

  Saturday, March 09, 2024

  SIMBA SC YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 MKWAKWANI


  SIMBA SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Coastal Unión katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Mabao ya Simba yamefungwa na washambuliaji wake wageni, Muivory Coast Freddy Michael Koublan dakika ya 11 na Mcameroon Willy Essomba Onana dakika ya 73, huku bao pekee la Coastal Unión likifungwa na kiungo mzawa, Lucas Almeida Kikoti dakika ya 24.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 39 katika mchezo wa 17, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 44 za mechi 20, wakati Coastal Unión inabaki na pointi zake 27 za mechi 20 sasa nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top