• HABARI MPYA

  Saturday, March 16, 2024

  TANZANITE YATUPWA NJE RASMI ALL AFRICAN GAMES


  TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imeaga rasmi Michezo ya Afrika (All Africans Games) baada ya sare ya kufungana bao 1-1 na Ethiopia katika mchezo wa mwisho wa Kundi A jana Uwanja wa Michezonwa Cape Coast nchini Ghana.
  Bao la Tanzania katika mchezo huo lilifungwa na Husnath Ubamba na kwa matokeo hayo Tanzanite inamaliza nafasi ya tatu ikivuna pointi mbili nyuma ya wenyeji, Ghana  iliyomaliza na pointi saba na Uganda pointi tano, wakati Ethiopia imeshika mkia kwa pointi yake moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YATUPWA NJE RASMI ALL AFRICAN GAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top