• HABARI MPYA

  Saturday, March 02, 2024

  LIVERPOOL YAICHAPA NOTTINGHAM FOREST 1-0 BAO LA JIONI KABISA


  BAO la dakika ya 90+9 la mshambuliaji wa Kimataifa wa Uruguay, Darwin Nunez limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa The City Ground, Nottingham, Nottinghamshire.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 63 katika mchezo wa 27 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao, Nottingham Forest wanabaki na pointi zao 24 za mechi 27 pia nafasi ya 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA NOTTINGHAM FOREST 1-0 BAO LA JIONI KABISA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top