• HABARI MPYA

  Thursday, March 07, 2024

  MAN CITY NA REAL MADRID ZATANGULIA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA UEFA


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamefanikiwa kwenda hatua ya Robó Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya FC Copenhagen usiku wa jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Manuel Akanji dakika ya tano, Julian Alvarez dakika ya tisa na Erling Haaland dakika ya 45 na ushei ambalo hilo linakuwa bao lake la 29 msimu huu huku bao la FC Copenhagen likifungwa na Mohamed Elyounoussi dakika ya 29.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City inakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 6-2 kufuatia kuwachapa FC Copenhagen 3-1 pia kwenye mchezo wa kwanza Denmark.
  Nao Real Madrid wametinga Robo Fainali pia licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 na RB Leipzig jana Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.
  Vinícius Júnior alianza kuifungia Real Madrid dakika ya 65, kabla ya Vilmos Orbán kuisawazishia RB Leipzig dakika ya 68.
  Real Madrid wanakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kuwachapa RB Leipzig 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Ujerumani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY NA REAL MADRID ZATANGULIA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA UEFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top