MABINGWA watetezi, Manchester City wamewadhibu mahasimu, Manchester United kwa kuwatandika mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Ni Manchester United waliotangulia kwa bao la Marcus Rashford dakika ya nane, kabla ya Manchester City kutoka nyuma kwa mabao ya Philip Foden dakika ya 56 na 80 na Erling Haaland dakika ya 90+1.
Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi 62, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi moja na Liverpool baada ya wote kucheza mechi 27, wakati Manchester United wanabaki na pointi zao 44 za mechi 27 pia nafasi ya sita.
0 comments:
Post a Comment