• HABARI MPYA

  Friday, March 29, 2024

  DIARRA, AZIZ KI, AUCHO NA PACOME WAMEFANYA MAZOEZI LEO JIONI KIGAMBONI


  KIPA Mmali, Djigui Diarra na viungo, Mburkinabe Stephane Aziz Ki, Mganda Khalid Aucho na Muivory Coast Peadoh Pacome Zouazoua wote wamefanya mazoezi jioni ya leo Uwanja wa Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kuekelea mchezo wa dhidi ya Mamelodi Sundowns.
  Kwa upande wake beki Muivory Coast, Kouassi Attohoula Yao alifanya mazoezi mepesi tu ya peke yake. 
  Leo mchana Kocha Muargentina wa Yanga SC, Miguel Ángel Gamondi akielezea hofu yake juu ya wachezaji hao akisema hajui kama atawatumia kwa sababu hadi leo asubuhi walikuwa hawajarejea kutoka kwenye majukumu yao ya timu za taifa.
  Pamoja na wawili hao, Gamondi pia alithibitisha atawakosa nyota wake wanne, mabeki Kibwana Shomari, Kouassi Attohoula Yao (Ivory Coast)na viungo Peadoh Pacome Zouazoua (Ivory Coast) na Khalid Aucho (Uganda) ambao wote ni majeruhi.
  Yanga watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kesho kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana  Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria.
  Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2001 na Mamelodi Sundowns wakaitoa Yanga kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 3-2 Pretoria na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mshindi wa jumla baina ya Yanga na Mamelodi Sundwons atakutana na mshindi wa jumla katí ya Esperance ya Tunisia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIARRA, AZIZ KI, AUCHO NA PACOME WAMEFANYA MAZOEZI LEO JIONI KIGAMBONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top