• HABARI MPYA

  Sunday, March 10, 2024

  WAZIRI JUNIOR APIGA HAT TRICK KMC YAICHAPA TABORA UNITED 4-2


  WENYEJI, KMC wameibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya KMC leo yamefungwa na Daruwesh Saliboko dakika ya 44 na Waziri Junior Shentembo matatu, dakika za 49, 60 na 67 huku mabao ya Tabora United yakifungwa na Daniel Lukandamila dakika ya 84 na la penalti dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 28 na kusogea nafasi ya nne, wakati Tabora United inabaki na pointi zake 21 nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 21.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI JUNIOR APIGA HAT TRICK KMC YAICHAPA TABORA UNITED 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top